25 Januari 2014 - 20:30
Ghala la silaha lalipuka Congo

Watu 20 wanahofiwa kufariki kutokana na mlipuko katika ghala la silaha katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Vikosi vya kulinda amani vya umoja wa mataifa nchini humo ,vimesema kuwa nyumba nyingi zilaharibiwa wakati wa mlipuko huo katika kambi moja ya kijeshi karibu na soko kuu la Mbuji-mayi.Mlipuko huo uliotokea katika mji wa Mbuji-Mayi inasemekana ulisababishwa na radi kali.Kwa mujibu wa taarifa za kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa Monusco,zaidi ya watu 50 pia walijeruhiwa huku nyumba kadhaa zikiharibiwa.askari wa kulinda amani kutoka umoja wa mataifa wanashirikiana na jeshi na wananchi wa Congo katika kusaidia waloathirika na tukio hilo.